KUHUSU ONPOINTGRAPHICS

Onpointgraphics ilianzishwa mwaka 2017 na Hafidhi Mitambo ambae alikuwa na lengo la kuhitaji watu wajifunze kwa kutumia lugha ya kiswahili kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu softwares za kompyuta pamoja na simu namna ya kuzitumia kwaajili ya kuleta matokeo katika nyanja mbalimbali.

Kwasababu aliamini kujifunza kwa kutumia lugha yako mama kunafungua nafasi kwa watu wengi zaidi kuweza kuelewa kwa urahisi kitu kinachofundishwa ukifananisha na kujifunza kwa lugha za kigeni ambazo inapelekea kukariri zaidi na kupata uvivu wa kusoma kinachofundishwa. Wakati inaanzishwa ilikuwa na kozi moja tu ambayo ilikuwa Design kwa kutumia simu (Canva), Lakini baada ya miaka saba tulifikia lengo letu na kuwa na kozi takribani 38+ katika platform tofauti tofauti.

Onpointgraphics inajihusisha na kutoa mafunzo ya kompyuta mtandaoni kwa lugha ya kiswahili, inatoa mafunzo ya kozi kama vile Graphics design, Video editing, motion design, microsoft office na Website design lakini pia kufanya kazi mbalimbali za Graphics design, Video Editing, Website design na motion design kwaajili ya watu binafsi, makampuni na taasisi mbalimbali.